Back to top

Wahitimu wa vyuo vikuu waandaliwe kujifunza ujasiriamali - SIMBEYE

18 May 2018
Share

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya sekta binafsi Tanzania (TPSF) GODFREY SIMBEYE Amewataka wakuu wa vyuo vikuu nchini kuhakikisha wanashirikiana kutoa mafunzo yatakayowezesha wahitimu kujifunza ujasiriamali ili waweze kujiajiri baada kuhitimu vyuo vikuu.

Akizungumza katika Kongamano la kambi ya Ujasiliamali lililoandaliwa na chuo kikuu cha Mzumbe mjini Morogoro Bwana SIMBEYE Amesema hatua hiyo itasaidia kupunguza idadi kubwa ya vijana wanaohitimu vyuo vikuu walioko mitaani wakisubiri ajira za serikali.

Bwana  SIMBEYE amesema kumekuwa na  changamoto kubwa ya wanafunzi kushindwa kujiajiri wanapomaliza masomo ya elimu ya juu hali inayoongeza  wimbi la vijana wasio na ajira.

Katibu tawala wa mkoa wa Morogoro,  akimwakilisha katibu mkuu wizara ya elimu,sayansi na teknolojia dk LEONARD AKWILAPO amesema mipango ya serikali nikuhakikisha wanaweka mazingira bora ya biashara hivyo ni vyema vijana hao kuwa wabunifu na kuboresha biashara zao.

Makamu mkuu wa chuo kikuu cha Sokoine cha kilimo -SUA- profesa, RAPHAEL CHIBUNDA ametaka wanafunzi hao kuwa na fikra za ujasiliamali mapema kwa kuanza kufikiria miradi iatakayosaidia kuwawezesha kujiajiri.