Back to top

Wahukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa mauaji ya kukata koromeo Kagera. 

13 August 2020
Share

Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba leo imewapa adhabu nyingine ya kunyongwa hadi kufa watu wawili waliokuwa wanakabiliwa na tuhuma kuwaua watu na kisha kuwakata watu makoromeo pamoja na uchomaji wa makanisa ya madhehebu ya kikiristo baada ya kupatikana na hatia ya kumuua kikatili Herman Diligi Mkazi wa Kagemu.

Hukumu hiyo imetolewa na Jaji wa Mahakama kuu ya Tanzania Sam Rumanyika na waliopewa adhabu ya kunyonywa hadi kufa ni Alyu Dauda na Rashid Mzee Ali na katika kesi hiyo mahakama imemuachia huru Ngesela Kea  Joseph kwa kile kilichoelezwa kuwa ushahidi uliotolewa dhidi yake haukumtia hatiani .

Adhabu ya kunyongwa hadi kufa iliyotolewa kwa watu wawili kujihusisha na vitendo vya kuwaua na kuwakata makoromeo ni ya pili, adhabu ya kwanza ya aina hiyo ilitolewa na Mheshimiwa Jaji Michael Mlacha kwa watu wote watatu baada ya kupatikana na tuhuma ya kuwaua watu wanne wakazi wa Katoma kwa kuwakata makoromeo pia wameishapata adhabu nyingine za vifungo vya maisha kwa kuchoma makanisa ya madhehebu ya kikiristo.

Mahakama hiyo pia imempa adhabu ya kunyongwa hadi kufa, Shija Bunzali baada ya kupatikana na hatia ya kumuua kikatili aliyekuwa diwani wa kata ya Kimwani kwa tiketi ya CUF , Sylverster Faustine.