Back to top

WAHUSIKA UDANGANYIFU WA MITIHANI KUBANWA

17 May 2022
Share

Serikali imesema itaendelea kuwachukulia hatua kali kwa mujibu wa sheria wahusika wote wanaojihusisha na udanganyifu wa mitihani ili kuhakikisha kuwa taifa linapata wataalam wenye sifa stahiki.

Hayo yamesemwa Bungeni na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe.Omary Kipanga alipokuwa akijibu swali la Mhe.Husna Juma Sekiboko (Viti Maalum) aliyetaka kujua Serikali inachukua hatua gani kukomesha kuvuja kwa mitihani nchini.

Mh.Kipanga akaongeza kuwa Serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kwa lengo la kukomesha tabia ya udanganyifu katika mitihani  ya Taifa ikiwemo mitihani ya kumaliza Elimu ya Msingi, Sekondari na Vyuo.

Ameongeza kuwa hatua hizo ni pamoja na kutoa elimu kwa walimu, wasimamizi wa mitihani na wadau wote wa elimu kuhusu athari za udanganyifu katika mitihani ili kuhakikisha kuwa wanatekeleza jukumu la usimamizi wa mitihani hiyo kwa uadilifu.