Back to top

WAIBIA WATU WAKIDAI NI FEDHA ZA KUJENGEA MSIKITI

07 April 2024
Share

Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Mkoa wa Tabora, limeiomba serikali kufanya oparesheni ya kuwasaka na kuwachukulia hatua za kisheria baadhi ya vijana wanaopita mitaani na kutapeli watu, kwa kukusanya fedha kinyume na utaratibu wakidai ni michango ya kujenga nyumba za ibada, hususani misikiti.
.
Baraza hilo limetoa ombi hilo baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wakazi wa Mkoa huo, juu ya adha hiyo, ambapo mmoja wa wajumbe wa Baraza hilo amesema kuwa, sadaka ya dini hiyo hukusanywa kwenye maeneo maalumu, kulingana na maelekezo ambayo Baraza hilo limetoa na si mitaani.