Back to top

Waziri Mkuu asema serikali haitafumbia macho utendaji usioridhisha.

30 January 2020
Share

Waziri Mkuu, Mhe.Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kukemea utendandaji usioridhisha pale inapoona mambo hayaendi sawa katika maeneo mbalimbali nchini pamoja na Zanzibar.

Amesema maagizo aliyoyatoa tarehe 18 mwezi huu alipotembelea kiwanda cha sukari cha Zanzibar kilichopo Mahonda, wilaya ya Kaskazini 'A', mkoa wa Kaskazini Unguja ni sahihi kwa kuwa yanalenga kuboresha maendeleo na kulinda wawekezaji.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Baraza la Wawakilishi, Mhe.Jaku Hashimu Ayoub katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu.

Mbunge huyo alitaka kufahamu ni lini Serikali itaruhusu sukari inayo tengenezwa na kiwanda cha Sukari Zanzibar iuzwe Tanzania Bara.

Waziri Mkuu amesema mpango wa uagizaji sukari kutoka nje ya nchi hauko sahihi, kwani wanunuzi walitakiwa kwanza wanunue sukari inayo tengenezwa ndani ndipo waagize nje kiasi kinachopungua.