Back to top

Wajasiriamali mkoani Mwanza wahimizwa kuboresha biashara zao.

17 September 2019
Share

Wajasiriamali na wafanyabiashara mkoani Mwanza wamehimizwa kuzitumia fursa zilizopo mkoani humo kwa kuzibadilisha na kuziboresha ili ziweze kuleta tija na kubadilisha hali zao kiuchumi.

Rai hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Nyamagana Dkt. Philis Nyimbi aliyemwakilisha mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella katika ufunguzi wa kongamano la mafunzo kuhusu mbinu mbalimbali za kibiashara na fedha kwa wajasiliamali zaidi ya 300.

Bibi Anastazia Mkono ni mmoja kati ya washiriki katika kongamano hilo pia mfanyabiashara katika soko la mitumba mlango mmoja  anasema kwamba wafanyabiashara wengi wanashindwa kufikia malengo yao kutokana na kutokuwa na mbinu za kibiashara na jinsi ya kulipa mikopo wanayokuwa wameikopa