Back to top

WAJITOSA BWAWANI BAADA YA KUDAIWA KUBAKA

20 June 2023
Share

Watu wanne ambao hawajafahamika wamejitosa kwenye bwawa la maji la Kitaji, lililopo Manispaa ya Musoma, mkoani Mara, ambalo lina kina kirefu cha maji na tope, baada ya kudaiwa kumbaka mwanamke mwenye umri wa miaka 35 (jina limehifadhiwa), kisha kumjeruhi kwa kumchoma na visu katika maeneo mbalimbali ya mwili wake.
.
Akizungumza kufuatia tukio hilo, Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji, Mrakibu Agustine Magere, amesema walifika eneo la tukio baada kupata taarifa, ambapo waliwatafuta watu hao bila mafanikio.