
Wajumbe wa Mkutano wa Kamati Tendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), wamewasili nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.
Wajumbe hao wanatarajiwa kushiriki Mkutano huo utakaofanyika Februari 13, 2026, katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo utaongozwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Dkt. Patrick Motsepe, na unatarajiwa kukutanisha viongozi mbalimbali wa soka barani Afrika kujadili masuala muhimu ya maendeleo ya mpira wa miguu.
Uenyeji wa mkutano huo unaendelea kuonesha nafasi ya Tanzania katika ramani ya soka la Afrika, hususan katika kipindi hiki cha maandalizi ya mashindano ya AFCON 2027.
