Back to top

Wakazi 11 wafariki kwa kuangukiwa ukuta na kusombwa na maji Morogoro.

16 May 2020
Share

Watu 11 wa vijiji viwili tofauti wamefariki dunia  kutokana na mvua zilizonyesha usiku mmoja wa kuamkia Ijumaa, wanne kati yao wa familia moja kwa kuangukiwa na ukuta na wengine saba kwa kusombwa na maji yaliyoingia kwenye nyumba zao wakati wamelala usiku wa manane, yakitokea milimani huko kijiji cha Pemba, kata ya Pemba wilayani Mvomero.


Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro SACP Wilbroad Mutafungwa amesema tukio la  familia moja ya watu wanne kuangukiwa na ukuta, limetokea kijiji cha Konde, tarafa ya Matombo wilayani Morogoro.


Kuhusu waliokufa maji, SACP Mutafungwa amesema kati ya watu saba waliofariki dunia, watano ni watoto wadogo wa umri wa kati ya miaka 6 hadi 14, sambamba na mtoto mwingine mchanga ambaye bado alikuwa hajapewa jina.