Back to top

Wakazi 33 waliounguliwa nyumba zao waanza kupata msaada, DC aeleza.

10 September 2019
Share

Mkuu wa wilaya ya Tunduru Bw.Julius Mtatiro akizungumza kwa njia ya simu amesema kuwa serikali inafanya kila liwezekanalo kuwasaidia wakazi 33 waliokumbwa na janga la nyumba zao kuungua moto Tunduru mkoani Ruvuma. 

Amesema kwa sasa watu waliokosa mahala pa kusihi kutokana na mkasa huo wamehifadhiwa kwa majirani na kwamba misaada ya vyakula imeshaanza kupelekwa huku kukiwa na mipango ya kuziezeka nyumba zao zilizoteketea kwa moto na bati zimeshaanza kuwasili kwa waliokumbwa na maafa hayo.

Kufuatia tukio hilo kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma ACP Simon Maigwa Marwa amewataka wananchi kuwa makini wanapoaandaa mashamba yao kwa kuchoma moto mashamba ili kuepuka madhara makubwa kama hili lililojitokeza katika kijiji cha Huria tarafa ya Matemanga wilayani Tunduru mkoani Ruvuma.

Kutokana na tukio hilo la wakazi nyumba zao kuungua moto na kusababisha kukosa makazi limesababisha Mtoto Fitina Tukolyese mkazi wa Tunduru mkoani humo kufariki huku babu yake akilazwa katika kituo cha afya Nakapanya baada ya kuungua alipokuwa akijaribu kuokoa maisha ya mjukuu wake huyo.