Back to top

WAKAZI IRINGA WATUNZE MIRADI YA MAENDELEO.

12 August 2022
Share

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan, amewataka wakazi wa mkoa wa Iringa kuitunza miradi ya maendeleo ambayo imeanzishwa na Serikali mkoani humo.

Rais Samia amesema hayo wakati akiweka jiwe la msingi la upanuzi wa uwanja wa ndege wa Iringa,  na kuongeza kuwa miradi hiyo ya maendeleo imelenga kukuza uchumi wa mkoa huo na taifa kwa ujumla.

Aidha Mhe.Rais amewataka wakazi wa mkoa huo kufanya kazi kwa bidii katika Nyanja zote zikiwemo kilimo na biashara ili ziwawezeshe waweze kuwa na maisha bora.

Mradi huo wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Iringa unajengwa kwa fedha kutoka benki ya dunia na Serikali ya Tanzania.

Rais Samia yupo ziarani mkoani Iringa.