Back to top

Wakazi wa Kijiji cha Ngoma, Sengerema wajengewa kituo cha polisi.

02 May 2021
Share

Zaidi ya wakazi 11,000 wa kijiji cha Ngoma kata ya Igalula wilayani Sengerema mkoani Mwanza ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa kituo cha polisi katika kata hiyo na kulazimika kutembea umbali wa zaidi ya kilomita 30 kufuata huduma hiyo katika kijiji cha Buyagu, hatimaye wamejengewa kituo cha polisi kilichogharimu shilingi milioni 45 hadi kukamilika.
.
Wananchi hao baada ya kukabidhiwa jengo hilo la kituo cha polisi kilichojengwa na mwekezaji wa kampuni uchimbaji madini ya ORE CORP, wamesema  kituo hicho cha polisi kitawasaidia katika ulinzi na usalama wa mali zao. 
.
Aidha, Afisa mahusiano wa kampuni hiyo Bw.John Bwana, akikabidhi kituo hicho kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella aliyewakilishwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Sengerema, Bw.Allan Augustine, amesema ujenzi wa kituo hicho cha polisi ni moja kati ya miradi 30 ya kuiendeleza jamii kabla ya kuanza uchimbaji wa madini katika mgodi wa Nyanzaga.