Back to top

Wakazi wa Mwakitolyo,Shinyanga wahofia kukosa mawasiliano ya barabara

10 December 2018
Share

Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu katika eneo la Mwaktolyo wilaya ya Shinyanga , Mkoani Shinyanga wameingiwa na hofu ya kukosa mawasiliano ya barabara baada ya barabara iliyosombwa na mvua katika msimu wa mvua uliyopitwa kutengenezwa bila kuwekewea kalavati na madaraja ya kupitisha maji ya mvua.

Wachimbaji hao wamesema  mvua za vuli zinazoanza kunyesha katika maeneo mengi nchini zinaweza kuwafanya waishi kisiwani kwa kukosa mawasiliano ya barabara .

Hata hivyo, kaimu meneja wa TANROADS Mkoa wa Shinyanga Mhandisi MIbara Ndirimbi amesema barabara hiyo ipo katika hatua ya kwanza ya marekebisho na kuwa bado barabara hiyo inafanyiwa marekebisho ili kuepuka changamoto ya mafuriko. 

Kwa upande Wake Naibu Waziri wa ujenzi Mh.Elias Kwandikwa amesema barabara hiyo inayotoka Kahama kupitia Mwakitilyo hadi Shinyanga ipo katika mpango wa kujengwa katika kiwango cha lami.