Back to top

Wakazi wa Tanga wamehadharishwa na Ugonjwa wa Dengue.

31 March 2018
Share

Wakazi wa jiji la Tanga wamehadharishwa kuwa wanapohisi kuwa na homa kali waende haraka katika kituo cha afya au hospitali iliyopo karibu kwa ajili ya vipimo na matibabu kufuatia mgonjwa mmoja kutoka Kenya kuingia nchini akiwa mgonjwa na alipopimwa alibainika kuwa na ugonjwa wa Dengue.

Mganga Mkuu wwa jiji la Tanga Dakta JERY KANGA amesema mara baada ya kubaini kuwa mgonja huyo anaugua Dengue waliwahi kumpatia tiba na alipopata nafuu walimrudisha nchini Kenya ili kuepuka maambukizi kwa sababu yanatokana kwa njia ya virusi vitokananvyo na Mbu.

Katika hatua nyingine, wafugaji waishio mpakani mwa Kenya na Tanzania wameiomba serikali kuingilia kati kufuatia baadhi ya viongozi wa serikali za vijiji kuuza mashamba ya wenyeji kwa Wakenya kitendo ambacho kinaweza kusababisha migogoro baina ya pande hizo mbili.

Wafugaji hao wameiomba serikali kukomesha migogoro ya ardhi kwa sababu mifugop yao haina mahali pa kunywesha mifugo yao kwani bwawa walilokuwa wakilitegemea limebomolewa na maji ya mvua.