Back to top

Wakimbizi kupata chanjo ya UVIKO -19 – Katavi.

02 August 2021
Share

Serikali imeanza utaratibu wa kuhesabu idadi ya wakimbizi na wakazi  kutoka katika kambi na makazi mbalimbali ya wakimbizi hao  ambao wamekubali kuchanjwa chanjo ya kuzuia ugonjwa wa Virusi vya Corona.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo ametoa taarifa hiyo  alipotembelea Kituo cha Afya cha Katumba kilichopo katika Makazi ya Wakimbizi Katumba ambayo yanahifadhi wakimbizi 86,233 ambao wako nchini toka Mwaka 1972baada ya kukimbia machafuko ya kikabila  nchini Burundi.