Back to top

WAKINAMAMA 100 HATIANI, KWA KUTUMA WATOTO KUOMBA.

23 February 2024
Share

Zaidi ya akinamama 100 wa Karamojong, Kampala nchini Uganda, wamenusurika kifungo cha kwenda jela, na badala yake wamehukumiwa kufanya kazi za kijamii baada ya kukutwa na hatia ya kuwatuma watoto wao katika mitaa tofauti ya mji mkuu wa mtaa wa Kampala kuombaomba.

Hakimu wa Mahakama ya Jiji la Darasa la Kwanza Edger Karakire, angeweza kumhukumu kila mwanamke kifungo cha miezi sita, lakini badala yake, aliwahukumu kifungo cha mwezi mmoja katika huduma ya jamii kila mmoja katika wilaya yao ya Napak.

Jaji huyo amesema uamuzi wake huo unalengo la kuwapa akinamama hao nafasi nyingine ya kujirekebisha.

Kundi hilo sasa limerudishwa Karamoja kukamilisha adhabu yao ambayo hakimu wa kesi alisema itanufaisha jamii zao.