Back to top

Wakulima tumieni mbegu bora zilizofanyiwa utafiti.

25 June 2022
Share

Wakulima wa zao la mpunga katika Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameshauriwa kutumia mbegu bora zilizofanyiwa utafiti na taasisi zenye mamlaka ili kuepuka kupata mavuno hafifu na yasiyo na tija.

Ushauriwa huo umetolewa na wadau wa zao la mpunga kutoka katika Taasisi ya Utafiti wa Mbegu za Mpunga Duniani (IRRI) pamoja na wataalamu wa kilimo wa Halmashauri ya Ushetu wakati wakitoa elimu kwa vitendo mashambani kwa wakulima kwenye kijiji cha Mpunze kilichoko katika Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama.