Back to top

Wakulima wa chai Lupembe wamuomba rais Magufuli kuwasaidia kulipwa

09 January 2019
Share

Wakulima wa zao la chai kutoka vijiji vya Igombola,Mfiliga,Idamba tarafa ya Lupembe mkoani Njombe wamemuomba rais Dkt.John Magufuli kuingilia kati mgogoro uliopo kati ya chama cha muungano wa vyama vya ushirika vya wakulima wa zao la chai-Lupembe(MUVYULU) na mwekezaji wa kiwanda cha chai cha Igombola(Mullah) ambaye ameshindwa kuwalipa wakulima wa chai zaidi ya shilingi milioni mia moja  hadi sasa.

Wakulima hawa wametoa kilio chao mbele ya naibu waziri wa kilimo na umwagiliaji nchini Mhe.Innocent Bashungwa katika kijiji cha Igombola tarafa ya Lupembe kufuatia kutolipwa kwa fedha zao tangu mwezi mei mwaka jana,ambapo imepelekea baadhi yao kushindwa kuwapeleka watoto shule.