Back to top

Wakulima wa Korosho Mtwara watakiwa kufuata ushauri wa wataalamu.

13 August 2019
Share

Taasisi ya utafiti wa kilimo TARI naliendele kanda ya kusini imewataka baadhi ya wakulima wa zao la Korosho wa mikoa ya Mtwara na Lindi kufuata ushauri wa wataalamu ili kudhibiti kiwango kikubwa cha unyevu nyevu kinachojitokeza kwenye korosho baada ya kuvunwa na hivyo kukosa soko.

Kauli hiyo imetolewa na mtafiti kiongozi wa zao la Korosho kutoka taasisi ya utafiti wa kilimo TARI naliendele Dkt.Fortunatus Kapinga katika mahojiano ITV.

Amesema kwa mujibu wa wataalamu kiwango cha unyevu nyevu kinachokubalika kwenye zao la Korosho kisizidi asilimia kumi, zaidi ya hapo zao hilo linaweza kuharibika na kukosa soko hivyo mkulima kupata hasara.

Amesema katika kipindi hiki ambacho wakulima wako katika hatua ya kupalilia mikorosho ni vema wakatambua njia sahihi za kutunza korosho mara baada ya kuzivuna ikiwa ni pamoja na kuzianika, kuzitunza kwenye magunia ambayo yatawekwa juu ya mbao na si kuwekwa kwenye sakafuni.

Ameabainisha kuwa hatua hizo zitasaidia kupunguza idadi kubwa ya korosho zinazokataliwa kwenye maghala kutokana na kuwapo kwa utunzaji mbovu kutoka kwa baadhi ya wakulima wa zao hilo na hivyo kupata hasara.