Back to top

Wakulima wa Korosho wataka kudhibitiwa bandari bubu.

17 October 2020
Share


Wakulima wa korosho wa kata ya Mkonona wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara wameiomba serikali idhibiti bandari bubu zilizo kwenye kata hiyo, ili kukomesha uingiaji holela wa watu, kitendo kinachotishia usalama wao.

Wametoa ombi hilo kwenye mnada wa pili wa korosho ulioandaliwa na Chama Kikuu cha Ushirika cha Masasi /Mtwara na MAMCU, baada ya kupewa fursa ya kueleza changamoto zinazowakabili.

Akizungumza na wakulima na wananchi wengine waliohudhuria mnada huo, Mkuu wa Wilaya ya Nayumbu Bwana Moses Machali amesema, serikali inatambua na changamoto hiyo na ipo macho kukabiliana na wanaojihusisha na usafirishaji wa wahamiaji haramu.

Akitoa taarifa yam nada huo, Meneja wa MAMCU Pontency Rwiza amesema wakulima wameridhia kuuza korosho zao kwa bei ya shilingi elfu mbili mia nne hamsini na tisa kwa kilo moja ambayo ni ya juu na shilingi elfu mbili mia mbili arobaini na nane bei ya chini.

Kwa upande wao, wakulima wametaka walipwe fedha zao haraka.