Back to top

Wakulima wa muhogo Handeni waomba kuwekewa bei elekezi.

23 February 2020
Share

Wakulima wa zao la muhogo wilayani Handeni mkoani Tanga wameiomba serikali kuweka bei elekezi ya zao hilo  kama ilivyo kwenye zao la korosho ili kuwabana wanunuzi holela  ambao husababisha wakulima kutokuona faida ya kilimo cha zao hilo.


Wakati mkuu wa wilaya ya Handeni  Godwin Gondwe anaanzisha mkakati wa zao hilo lengo kubwa ilikuwa ni kukabiliana na njaa lakini mwitikio umekuwa ni mkubwa na hivyo imepelekea wakulima hao kuomba kutafutiwa masoko baada ya kuonekena muhogo umekuwa ni mwingi .