Back to top

Wakulima wa zao la alizeti washauriwa kutumia mbegu za SDC 36.

20 August 2018
Share

Wakulima wa zao la alizeti katika mikoa ya lindi na mtwara, wameshauriwa kutumia mbegu za SDC 36 pamoja na 145 kutokana na mbegu hizo kustahamili ukame na magonjwa.

Ushauri huo umetolewa na afisa kilimo kutoka mradi unahusika na masuala ya usambazaji, uelimishaji na uhamasishaji kilimo cha alizeti SDC, Bw.Solomon Niclaus.

Kwa upande wao baadhi ya wakulima wa zao la alizeti ambao tayari wamshaanza kunufaika kwa kuuza mafuta ya alizeti wakawashauri wakulima wenzao kuona umuhimu wa kujiunga kwenye vikundi ili waweze kusaidiwa kwa haraka pindi wanapokuwa kwenye vikundi hivyo.