Back to top

Wakulima wadogo watakiwa kutojali maslahi binafsi

09 December 2019
Share

Wakulima wadogo nchini wametakiwa kudumisha umoja badala ya ubinafsi kwa kuzingatia  misingi ya kujikomboa na umaskini na kuenzi mchango wa waasisi wa taifa waliohamasisha umoja na kupigania uhuru bila kujali maslahi yao binafsi.
 
Hayo yameelezwa na baadhi ya viongozi wa mtandao wa vikundi vya wakulima nchini MVIWATA,wakati wakizungumza na wakulima wadogo zaidi ya 170 kutoka mikoa mbalimbali nchini waliokuwa wakijifunza masuala ya mtandao huo na uongozi ili kupata ubunifu zaidi hasa kwenye kilimo na kuwaelimisha wengine.