Back to top

Wakulima waiomba TAKUKURU kusimamia mizani za Korosho.

23 September 2018
Share

Wakulima wa zao la Korosho katika wilaya ya Tandaimba mkoani Mtwara wameiomba taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU kuwa sehemu ya kusimamia upimaji wa korosho za wakulima katika maghala makuu maeneo ambayo idadi kubwa za kilo za korosho hupotea katika kipindi hiki cha msimu wa mauzo ya korosho.

Wakizungumza katika mkutano uliyowakutanisha viongozi wa vyama vya ushirika wenye lengo la  kujiandaa na msimu wa korosho kwa mwaka 2018/2019 baadhi ya wakulima wamesema licha ya serikali kuweka mkazo katika hilo bado kunatatizo kwenye maghala makuu.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Tandaimba Sebastiani Wariyuba amesema kabla ya kuanza msimu watalamu wa mizani ni lazima wapite ili kuangalia kama ziko sawa ama zinachangamoto.