Back to top

Wakulima walia na bei kubwa ya mbegu za Alizeti

22 May 2018
Share

Wakulima wa zao la Alizeti katika wilaya ya Ruangwa kata ya Nandagala wamelalamikia bei kubwa ya mbegu za zao hilo ambalo limeonyesha kufanya vizuri katika wilaya hiyo, na hivyo kupelekea vikundi 17 vilivyoundwa kwa ajili ya uzalishaji kufa na kubaki vitano pekee.

Kauli hiyo imetolewa na afisa maendeleo ya jamii kata ya Nandagala Hilda Nyandoa baada ya kutoa kilio hicho kwa wataalamu na viongozi wa wilaya waliotembelea shamba darasa la zao la Alizeti katika kata hiyo.

Hata hivyo akizungumza katika mkutano uliyohusisha wakulima wa zao la Alizeti kutoka kata mbali mbali Mwenyekiti wa chama cha wasindika mafuta ya Alizeti Tanzania Ringo Iligo amekiri nchi kuwa na uhaba mkubwa wa mbegu bora, huku mkuu wa wilaya ya Ruangwa Joseph Mkirikiti akiwaasa wananchi wa wilaya hiyo kuchangamkia fursa ya kilimo hicho.