Back to top

Wakulima wilayani Namtumbo walalamika kuibiwa Korosho

23 March 2019
Share

Baadhi ya wakulima wa Korosho katika kijiji cha Lukusanguse, halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma, wamewalalamikia viongozi wao wa chama cha ushirika cha Mjimwema wakiwatuhumu kuchezea mizani na kuiba Korosho zao huku pia wakidai kiasi cha fedha zao walizopaswa kulipwa wamejiingizia kwenye akaunti zao kwa lengo la kujinufaisha.

Wakitoa malalamiko hayo kwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Bi. Christina Mndeme aliyetembelea kijiji hicho kwa lengo la kusikiliza kero mbalimbali za wananchi, wakulima hao wamesema kutokana na hujuma hizo walizofanyiwa na wengi wao kutopata fedha zao inakwamisha kuendelea na shughuli zao mbalimbali za maendeleo ikiwemo kupeleka watoto shule.

Kufuatia malalamiko hayo, mkuu huyo wa mkoa wa Ruvuma, Bi.Christina Mndeme akalazimika kutoa maagizo kwa mkuu wa wilaya ya Namtumbo, Bi. Sophia Kizigo kufuatilia malalamiko ya wakulima hao na kisha kuwakamata wote waliohusika kuwaibia wakulima fedha na Korosho zao.