Back to top

Wakurugenzi wa Halmashauri wanao wabugudhi wafanyabiashara waonywa.

12 April 2018
Share

Serikali imewaonya wakurugenzi wa halmashauri nchini ambao bado wanaendelea kuwatoza kodi za manyanyaso wafanyabiashara kuwa watachukuliwa hatua za kinidhamu.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais - Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Josephat Kandege amesema hayo Bungeni mkoani Dodoma wakati akijibu maswali yaliyoelekezwa kwa wizara hiyo.

Amesema Serikali haiwezi kuvumilia kuona agizo la Rais Dr.John Magufuli likipuuzwa kwa kuwa limelenga kuwapunguzia kero wananchi hasa wa hali ya chini.

Mapema bungeni hapo, Wabunge waliihoji Serikali kuhusiana na kuendelea kusumbuliwa kwa wafanyabiashara wadogowadogo kwa kutozwa ushuru kinyume na agizo la Rais Magufuli.