
Katibu Mkuu TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe amewashusha vyeo na kuwapangia majukumu mengine wakuu wa vitengo vya manunuzi 23 ambao wamethibitika kuwa utendaji kazi wao haukuwa kuridhisha.
.
Hatua hiyo inafuata baada ya kufanyika kwa tathmini ya utendaji kazi kwa baadhi ya wakuu wa idara na vitengo kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa iliyoelekezwa na Mh. Rais Samia Suluhu Hassan wakati akiwa ziara mkoani Mara ambapo baada ya tathmini hiyo Waziri wa TAMISEMI Mhe. Innocent Bashungwa akamuelekeza Katibu Mkuu kuwashusha vyeo wakuu hao vitengo.


