Back to top

Wakuu vyuo vya elimu watakiwa kukabiliana ufaulu wa chini wa walimu.

10 January 2021
Share

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Tekinorojia Dkt.Leonard Aqwilapo amewataka wakuu wa vyuo vya elimu nchini kuhakikisha wanasimamia upatikanaji wa elimu bora ili kukabiliana na ufaulu wa chini wa waalimu ambao hauwezi kuzalisha wanafunzi bora kutokana na kufeli katika chuo.
 
Dkt.Leonard Aqwilapo ametoa agiizo hilo wakati akizungumza na wakuu wa vyuo vya ualimu na wakufunzi kutoka kanda ya kati, kanda ya ziwa na kanda ya magharibi wakiwa katika chuo cha ualimu mkoani Tabora ambapo amesema kuwa, ufaulu duni unatia shaka katika upatikanaji wa elimu bora.
 
Aidha katika hatua nyingine Dkt.Aqwilapo akizungumzia mkakati wa serikali kuwa na msingi bora wa ufundishaji amesema serikali itahakikisha vyuo vyote vya elimu vikiwemo vya serikali na binafsi viwe na mfumo bora wa ufyundishaji kwani wataliaandaa taifa moja.
 
Awali mkurugenzi mkuu wa taasisi ya elimu nchini Dkt.Annethy Komba akizungumzia uandaaji wa mafunzo kwa wakuu wa vyuo vya ualimu amesema serikali inatambua umuhimuwa mafunzo kazini na hivyo yataongeza utendaji kazi bora wa wakuu wa vyuo nchini.