
Waziri wa TAMISEMI Mh. Innocent Bashungwa amesema kuwa Wakurugenzi wa Halmashauri na Wakuu wa Wilaya watapimwa kutokana na utendaji kazi wao wa kuhakikisha wanatatua kero za wananchi, ambapo amebainisha kuwa moja ya kigezo kitakachotumika kuwapima ni kasi ya ukusanyaji wa mapato katika Halmashauri.
