Back to top

WALIJARIBU KUWAWEKEA MIHADARATI WANANGU - KENYATTA

24 July 2023
Share

Rais mstaafu wa Kenya, Uhuru Kenyatta, amedai kuwa serikali ya nchi hiyo ilijaribu kuwawekea watoto wake wawili wa kiume, Jomo Kenyatta na Muhoho Kenyatta, dawa za kulevya na bunduki katika makazi yao ili iwakamate na kuwashtaki.
.
Kenyatta ameyasema hayo alipokutana na kuzungumza na wahariri wa vyombo vya habari katika makazi yake, yaliyopo Jijini Nairobi, ambapo amelaani kitendo hicho huku akibainisha kuwa yeye alishajiondoa kwenye siasa na hafai kuhusishwa na maandamano ya upinzani yanayoendelea nchini humo.
.
Aidha, Kenyatta amebainisha kuwa watoto wake hawajapokea amri yoyote ya kusalimisha sialha zao kama ilivyodaiwa na serikali na vyombo vya habari, huku akidai kuwa watoto wake wawili, Jomo na Muhoho, ndio walikuwa na bunduki 6 pekee, na kwamba bintiye Ngina, hakuwa na silaha yoyote na kuongeza kuwa watoto hao walikuwa na leseni ya kumiliki silaha hizo kwa ajili ya kujilinda wao na familia zao.