
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Protas Mutayoba, amewataka walimu na wanafunzi kuwa mabalozi wazuri wa kukemea ukatili wa Kijinsia na unyanyasaji kwa watoto.



Kamanda Mutayoba ameeleza hayo alipofika shule ya Msingi Kisemvule, iliyopo Wilaya Mkuranga Kata ya Vikindu Mkoa wa Kipolisi Rufiji, wakati akitoa elimu ya ukatili wa Kijinsia na Unyanyasaji, ambapo amekemea vitendo vya ukatili vinavyofanywa na baadhi ya wazazi/walezi/walimu pamoja na wanafunzi ambavyo ni kinyume na sheria, huku akibainisha kuwa Jeshi hilo halitomuonea muhali mtu yeyote atakayebainika kuhusika na vitendo hivyo.
