Back to top

Walimu zaidi ya 170 wakusanyika kudai mafao yao Kigoma ujiji.

23 April 2018
Share

Zaidi ya walimu 170 wa shule za sekondari walio hamishwa kupelekwa kufundisha shule za msingi manispaa ya Kigoma ujiji wamelalamikia uongozi wa manispaa hiyo baada ya kutowalipa pesa za Uhamisho ya kutoka shule za sekondari kwenda shule za msingi kwa takribani miezi mitatu sasa.

Wakizungumza baada ya kukusanyika katika ofisi za Manispaa ya Kigoma ujiji kushinikiza kulipwa mafao yao, wamesema pamoja na kuhamishwa lakini hawajalipwa lakini pia wanahitaji mafunzo maalum ili kuweza kumudu kufundisha shule za msingi ambazo hawana maandalizi nayo.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma ujiji John Shauri amesema walimu hao hawawezi kulipwa posho ya usumbufu kwa kuwa wamehamishiwa katika shule ambazo ziko karibu na maeneo yao ya awali.