Back to top

Waliohusika na sakata la walimu kuchomwa mishale Iyogwe kusakwa.

27 June 2020
Share

Kutokana na habari zilizorushwa na kituo cha ITV kuhusu walimu sekondari ya Iyogwe kuchomwa mishale na kuuawa kwa mwalimu Madaraka Mganilwa na mwingine Hosea Charles kujeruhiwa, Jeshi la polisi mkoa wa Morogoro limeweka kikosi kazi maalum kikiongozwa na mkuu wa upelelezi mkoa na Ofisi ya Mkuu wa Polisi wilaya ya Gairo kwenye kijiji cha Chihwaga ilipo shule hiyo, ili kuwasaka wote waliohusika na matukio  hayo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Wilbroad Mutafungwa, amelazimika kukatiza ziara ya kikazi katika wilaya za Malinyi, Ulanga na Kilombero, na kwenda Gairo katika kijiji hicho, ambapo amebainisha kikosi kazi hicho kitafanya kazi usiku na mchana kuwabaini watuhumiwa wote wa matukio hayo ya kuua na kujeruhi.

 Tayari watuhumiwa wawili wako mahabusu na wengine waliotoroka wakiendelea kusakwa.