Back to top

Waliojiandikisha kupiga kura wachague viongozi wanaowataka -Wangabo

23 September 2020
Share


Mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amewataka watu wote waliojiandikisha kwa ajili ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu ujao waitumie kikamilifu fursa hiyo ili kuwachagua viongozi wanaowataka.

Aidha, amewakumbusha wakulima wasisahau kuandaa mashamba kwa ajili ya msimu ujao wakilimo, wakati huu wa kampeni za uchaguzi.

Aikagua miradi ya Lipa Kulingana na Matokeo na Miradi ya Afya na Usafi wa Mazingira na ujenzi wa madarasa na vyoo vya wananfunzi kwa shule za msingi na sekondari wilayani Kalambo, amesema mambo hayo mawili yanapaswa yaende pamoja kwa sababu mvua zinakaribia kunyesha.

Ametoa miezi miwili kwa halmashauri ya wilaya ya Kalambo kukamilisha miradi hiyo ili kuimarisha miundombinu ya shule hizo.