Back to top

Waliojifanya maofisa usalama wa Taifa Ikulu wakamatwa Mwanza.

07 January 2020
Share

Jeshi la polisi Mkoa wa Mwanza limewakamata watu 7 kwa tuhuma za kujifanya Maafisa wa Usalama wa Taifa kutoka Ikulu, na kuwatapeli wananchi na baadhi ya watumishi wengine wa serikali.

Kamanda wa polisi mkoani Mwanza Muliro Jumanne Muliro amewataka wananchi kutoa taarifa haraka polisi pindi wanapomtilia mashaka mtu yeyote ili hatua za haraka zichukuliwe.