Back to top

Waliomjeruhi kwa nondo Diwani Lindi kusakwa.

13 June 2022
Share

Jeshi la Polisi mkoani Lindi, linawatafuta watuhumiwa waliomjeruhi Diwani wa Kata ya  Navanga, Halmashauri ya Mtama, mkoani Lindi, Rashid Khalfan Mkuya, miaka 45, aliyejeruhiwa kwa kupigwa na kipande cha nondo sehemu mbalimbali za mwili wake, na kumsababishia majeraha kichwani na kifuani iliyopelekea kulazwa katika Hospitali ya Mission Ndanda, mkoani Mtwara kwa matibabu zaidi.

Kwa mujibu wa Kamishna Msaidi wa Jeshi la Polisi na Kamanda wa  Polisi mkoa wa Lindi ACP Mtatiro Kitinkwi, amesema tukio hilo limetokea tarehe 12/6/2022 majira ya saa tisa usiku, wakati diwani huyo  alipokuwa  anapambana na wezi  akijaribu kuokoa mali za mwanachi wake Ahmadi Ally Issa, aliyevunjwa duka lake na kuibiwa pesa kiasi cha shilingi 960, ooo.

Jeshi la polisi likishirikiana na wananchi wa vijiji jirani, linaendelea kuwatafuta watuhumiwa hao waliotumia pikipiki mbili aina ya TVS ambazo namba zake za usajili hazikufahamika.