Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana amewataka viongozi wa Chama hicho, kutokuwabeba wagombea au kupandikiza wagombea kwa njia yoyote ile, kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani.
.
Kinana ameyasema hayo wakati akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri iliyoboreshwa, Wilaya ya Serengeti, Mkoani Mara, ambapo amewakumbusha wanachama wa chama hicho kutenda haki katika uchaguzi huku akisisitiza kuwa kuchagua na kuchaguliwa ni haki ya kila mtu.
.
Aidha, Kinana amewaonya baadhi ya Viongozi ambao wamekuwa wakitoa rushwa kupata ili kupata Uongozi ambapo amesistiza kuwa vitendo vya rushwa vinasababisha kupata viongozi wanaoshindwa kuitumikia jamii.