Back to top

Wanafunzi 3 wafa maji wakiogelea mto Saghana

27 February 2022
Share

Wanafunzi watatu wa darasa la tano wa shule ya msingi Matala iliyopo Kata ya Mwika Kusini wilayani Moshi wamefariki kwa kuzama katika mto Saghana, ambapo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Simion Maigwa akabainisha kuwa wanafunzi hao ambao wawili kati yao ni mapacha waliamua kuogelea katika mto huo wakati wakirejea nyumbani, wakitokea shule.