Back to top

Wanafunzi Bariadi Simiyu waomba kambi za kitaaluma ziendelee.

14 April 2021
Share

Wanafunzi wa sekondari wilayani Bariadi mkoani Simiyu wamesema tangu kuanzishwa kwa kambi za kitaaluma mkoani humo mwaka 2017 hadi sasa  kumesaidia mkoa huo kufanya vizuri kielimu kutoka nafasi ya mwisho hadi kushika nafasi ya tatu kitaifa katika matokeo ya kidato cha sita mwaka jana .

Wakiongea na ITV katika shule ya sekondari Bariadi wanafunzi hao wamesema serikali iendelee na suala la kambi kwani zimeleta mabadiliko makubwa  kielimu.