Baadhi ya wanafunzi wanosoma katika shule za kata wilaya ya Musoma mkoa wa Mara wanadaiwa kujihusisha na biashara ya ngono kwenye Club nyakati za usiku huku wakijiita majina ya ‘mboga saba’ na ‘sex dadazi’.
Hayo yamebainishwa na na Mkuu wa wilaya ya Musoma Vicent Naano wakati akizungumza na wazazi kwa nyakati tofauti katika shule ya sekondari Nyabisare na Morembe ambazo wanafunzi wake 69 wamepata sifuri kati ya wanafunzi wanafunzi 217 waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana.
Akizungumza na ITV ofisini kwake ofisa elimu sekondari wilaya ya Musoma amekiri kuwepo kwa wanafunzi wanaofanya biashara ya ngono na kudai hali hiyo pia imesababisha matokeo ya kidato cha nne kubwa mabaya ambapo wilaya ya Musoma imeshika nafasi ya 139 kati ya halmashauri 185 kitafa.