Back to top

Wanafunzi Shule ya Msingi Namalombe wasomea chini ya mkorosho.

23 February 2021
Share

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Namalombe wilaya ya Nanyumbu mkoa wa Mtwara  na Mwalimu mkuu wao Bwanaheri Akili wameiomba serikali kuwajengea madarasa kwani kwasasa wanapata shida kusomea chini ya mkorosho kama darasa, kutokana na  shule hiyo kuwa na darasa moja tangu ilipoanzishwa mwaka 2014.

Naibu waziri wa TAMISEMI Mh. David Silinde akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Namalombe.


Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule hiyo  amesema wanafunzi wa darasa la saba, darasa la kwanza na darasa awali wanalazimika kusoma chini ya mkorosho huku darasa pili,la tatu,la nne, la tano na darasa la sita wote wakisoma katika jengo la darasa moja lililopo na kufanya kiwango cha kufundisha kuwa kidogo huku wakitumia choo  kimoja cha nyasi walimu na wanafunzi.

Darasa linalotumika na wanafunzi wa Shule ya Msingi Namalombe.


Hayo yamebainika baada  ya ziara ya Naibu waziri wa TAMISEMI David Silinde alipofika shuleni hapo baada ya kupata taarifa kuwepo kwa shule hiyo yenye darasa moja tu na kumuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa halmshauri wilaya ya Nanyumbu mkoa wa Mtwara Hamis Dambaya ndani ya miezi miwili wajenge madarasa manne haraka na kutenga katika bajeti ujenzi wa nyumba za walimu,ofisi na madarasa mengine huku yeye akihaidi atawapelekea madarasa matatu kutoka ofisi ya TAMISEMI.