
Wanafunzi wa shule ya awali Kibululu wilayani Iramba wanasomea nje wakiwa wamekaa chini wakituma miguu kama meza kwa kuandikia huku wakipigwa na jua,baridi na mvua inaponyesha hukatisha masomo,hali inayo wasababisha wanafunzi hao kukatisha ndoto zao za kupata elimu bora.
Mratibu Elimu kata wa Mgongo Bwana Lazaro Sakata pamoja na mkuu wa shule hiyo bi.Mwanjaa Mkoma wamesema hayo kwenye makabidhiano ya tani tano za saruji zilizotolewa na kampuni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya Mgongo Gold Mine ambazo zitatumika kuanzisha ujenzi wa madarasa ya wanafunzi wa darasa la awali.
Akikabidhi tani tano za saruji Mkurugenzi Mkuu wa Mgongo Gold Mine Bi.Herieth Sagati amesema wameamua kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais kwa kutaka wanafunzi kupata elimu wakiwa katika miundombinu bora,kwa kuchangia saruji ili kujenga madarasa ambayo yata waondolea adha ya kusoma nje wakiwa wamekaa chini wanafunzi wa shule ya awali ya msingi kibululu.
Shule hiyo ya msingi Kibululu ambayo ina wanafunzi wa darasa la awali mpaka la saba,inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo baadhi ya wanafunzi kuamua kufanya vibaya kwenye mitihani,kwa lengo la kufeli ili wafanye kazi kwenye machimbo ambayo yapo mengi wilayani Iramba .