Back to top

WANAFUNZI WAFARIKI KWA KUPIGWA NA RADI

03 March 2024
Share

Wanafunzi watatu wa shule ya msingi Kindimbachini na Shule ya Msingi Mapendano, zilizopo wilayani Mbinga, mkoani Ruvuma, wamefariki dunia, huku wengine 23 wakijeruhiwa, baada ya kupigwa na radi, wakati wakicheza kwenye mvua.
.
Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Bi.Aziza Mangosongo, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amewataka walimu kuhakikisha wanafunzi wanakaa madarasani wakati mvua zinanyesha, ili kuepuka madhara kama hayo.
.
Wanafunzi waliofariki kwenye tukio hilo ni Maria Hyera (8), Alfonce Hyera (8) na Deus Kayombo (8).