Back to top

WANAFUNZI WAPEWA ELIMU, UKATILI WA KINGONO NJOMBE

22 January 2023
Share

Jeshi la Polisi Kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto wilayani Njombe, limetoa elimu ya ukatili wa kingono kwa wanafunzi wa kike wa shule za sekondari wilayani humo.
.
Elimu hiyo imetolewa katika kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia lililowakutanisha wanafunzi wa kike kutoka shule 5 za serikali zilizopo mjini Njombe, lililoandaliwa na Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT).