
Serikali imezitaka Shule zote za Awali, Msingi, Sekondari na Vyuo vya Ualimu, kuendelea kutekeleza nyaraka na miongozo inayotolewa na Serikali, ikiwa ni pamoja na kuwapa wanafunzi haki ya kushiriki katika ibada kulingana imani zao, ili kupata matokeo bora katika utoaji wa malezi na elimu bora.
.
Hayo yamesemwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, kupitia taarifa iliyotolewa na Wizara hiyo kwenye mitandao yake ya kijamii, ambapo imebainisha kuwa maelekezo hayo ni kulingana na Waraka wa Elimu Na. 5 wa mwaka 1998 kuhusu somo la Dini, ambao pamoja na mambo mengine umesisitiza umuhimu wa mafunzo ya dini kwa wananfunzi ili kuwajengea maadili mema.

