Back to top

WANAFUNZI WARUDISHWA NYUMBANI KISA ABAYA

05 September 2023
Share

Shule za umma nchini Ufaransa zimewarudisha nyumbani baadhi ya wanafunzi wa kike kwa kukataa kuvua vazi lililopigwa marufuku maarufu kama Abaya ikiwa ni katika siku ya kwanza ya mwaka wa masomo.
.
Waziri wa Elimu Gabriel Attal amesema wanafunzi hao wamekaidi marufuku ya vazi hilo linaloonekana kuwa alama ya kidini, ambapo karibu wasichana 300 walienda shuleni Jumatatu asubuhi wakiwa wamevalia abaya wengine walikubali kubadilisha vazi hilo, lakini 67 walikataa na wakarudishwa nyumbani.
.
Serikali ilitangaza marufuku ya vazi hilo mwezi uliopita,  ikisema ilikiuka sheria za kutokuwa na udini katika elimu.