Back to top

Wanafunzi wawili wa familia moja wafa maji katika eneo la Chulwi.

15 May 2018
Share


Wanafunzi wawili wa familia moja Cuusin Twaha (7) na Fauha Twaha (5) wamekufa maji na watu wengine 10 kuokolewa katika eneo la Chulwi, Mkuranga.

Kwa mujibu wa Muandishi wetu wa #ITV ambaye amefika eneo hilo la Chulwi, Mkuranga ametueleza kuwa wanafunzi hao wawili waliokufa maji Cuusin Mwenye miaka 7 Darasa la Kwanza alimpitia mdogo wake wa miaka 5 anayesoma shule ya awali kurudi nyumbani ndipo walipoweza kupoteza maisha kwenye kivuko hicho ambacho kimetengenezwa kienyeji.

Amesema Maiti ilioonekana na kuopolewa ni ya Fauha Twaha mwenye miaka 5 mwanafunzi wa shule ya awali, huku juhudi za kutafuta mwili wa Cuusin Twaha mwenye miaka 7 zikiwa zinaendelea.

"Hiyo sehemu kuna kivuko watu wanavuka kienyeji sasa wanatumia magurudumu ya magari na miti kutengeneza tengeneza kama vingalawa tu vidogo vya kuvuka, lakini kutokana na mvua kubwa iliyoanza kunyesha usiku wa juzi kuamkia jana zimekuwa kubwa na kusababisha maafa hayo".Mwandishi wetu Ally Hengo ametueleza.

Ameongeza kwamba Katika tukio hilo watu kadhaa walikuwa wakivuka pamoja na wanafunzi ambapo watu wazima wameokolewa na wengine kujiokoa, lakini wanafunzi wawili mmoja amekutwa amekufa na mwili wake umepatikana leo na mwingine amesombwa na maji bado hajapatikana.

Kwa mujibu wa Mwandishi wetu wa #ITV Ally Hengo amesema Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji kimefika eneo la tukio kwa ajili ya kuutafuta mwili wa mtoto huyo ambaye bado haujapatikana.

Taarifa zaidi zitakujia.