Madaktari na Wauguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Tandahimba Mkoani Mtwara, wamewafanyia uchunguzi wa afya ya kinywa na meno na uwiano wa ubora wa lishe na uzito, wanafunzi wenye ulemavu wa akili kwenye shule maalumu ya Mji Mpya.
Baada ya uchuguzi huo wameshauri watoto wenye matatizo hayo, wasimamiwe kwa karibu katika utunzaji wa kinywa na meno ili kuwaepusha na magonjwa.
Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya hiyo, Daktari SILAS MBIKO amesema, watoto wenye ulemavu wa akili wanakabiliwa na hatari kubwa ya kupata magonjwa ya kinywa na meno kutokana na ulemavu huo .
Uchunguzi huo umekwenda pamoja na maandamano ya wauguzi, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Uuguzi Duniani, ambapo wananchi wengi na baadhi ya viongozi walijitokeza kuchangia damu kwa hiyari.