Back to top

Wanamgambo 52 wa Al-Shabaab wauawa na vikosi vya ulinzi vya Somalia.

22 February 2021
Share

Mkuu wa vikosi vya ulinzi vya Somalia Brigedia Jenerali Odowaa Yusuf Rageh ameiambia redio ya jeshi la taifa hilo kwamba, vikosi vya jeshi hilo vimefanikiwa kuwaua wanamgambo 52 wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab katika operesheni ya shambulio iliyofanywa dhidi ya ngome ya kundi hilo eneo la Shabelle ya Chini kusini mwa nchi hiyo.
.
Aidha, Jenerali Rageh ameongeza kuwa, katika operesheni hiyo, vikosi vya jeshi la serikali vimeteketeza pia maficho kadhaa ya magaidi wa Al-Shabaab.
.
Tangu mwaka 2007, kundi la kigaidi la Al-Shabaab limekuwa likiendesha kampeni ya mtutu wa bunduki kwa lengo la kuiangusha serikali kuu ya Somalia.
.
Mnamo mwaka 2011, kundi hilo la kigaidi lilitimuliwa katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu, kwa operesheni za pamoja za mashambulio zilizotekelezwa na jeshi la serikali likisaidiana na vikosi vya kijeshi vya Umoja wa Afrika( AMISOM).